Thursday, September 22, 2011

LIGI KUU YA TANZANIA IMEENDELEA


                                    
Katika uwanja wa Chamazi timu ya MORO United ilitoka sare ya magoli 2 kwa 2 katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam.

Dakika ya 35 goli la kwanza la JKT Ruvu lilifungwa Henry  Ngonye kabla ya JKT kusawazishwa na Husein Bunu katika dakika ya  67 kwa kuunganisha krosi ilipigwa na Rajabu Chau,

Dakika ya 79 Gaudience Mwaikimba aliifungia Moro goli la pili ambalo halikuweza kudumu na kusawazishwa katika dakika ya 81 ikiwa zimesalia dakika 9 t mchezo kumalizika,

Na kule mkoani Kagera, timu ya JKT Oljoro iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, dhidi ya Kagera Sugar, mechi iliyopigwa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Bao la kwanza la Oljoro lilifungwa na Amir Omari dakika ya nne, baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Kagera Sugar na kuukwamisha mpira wavuni.

Kwa mara nyingine JKT Oljoro ilijipatia bao la pili dakika ya 25, kupitia kwa mchezaji wake Omari kabla ya Kagera kupata bao la kufutia machozi katika dakika za mwisho za mchezo.

Kutoka mkoani Pwani, wapalianda wa Ruvu Shooting wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya African Lyon, kwenye Uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani.

Bao la kwanza la Ruvu Shooting lilifungwa katika dakika ya  28, kupitia kwa Kassim Linde na bao la pili la washindi lilipachikwa wavuni katika dakika ya 89, na Abrahman Abrahman.