Monday, August 22, 2011

FARBEGAS MWANZO MZURI




Kiungo wa mpya wa FC Barcelona Cesc Farbegas jana amefuwafurahisha mashabiki wake wa klabu hiyo ya Catalunya baada ya kufunga goli lake la kwanza tangu ajiunge na klabu hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Napoli 

Farbega amesema kwa sasa anamatumaini mapya juu ya ujio wake katika klabu hiyo aliyoitumikia wakati wa utoto wake na kusema atatomsaada wa kutosha kama alivyosaidiwa yeye klabu hiyo.

Hii inadhihirisha kuwepo mianya ya mafanikio kwa nyota huyo kwakua tangu ajiunge na klabu hiyo  amepata mafaniki kwa kutwaa mataji mara mbili.

Ambapo masaa 24 tangu ajiunge ametwaa taji la Super cup dhidi ya Real Madrid na usiku wa jana walitwaa  taji la hisani la Joan Gamper.

Siku ya Ijumaa kule Monaco nchini Ufaransa, Barcelona itaavaana na  Porto FC katika mchezo wa Super cup.

MAN UNITED YAINYUKA TATU BILA TOTTENHAM.


Manchester united yafanya mauaji ya pili baada ya kuibanjua  Tottenham kwa mabao matatu kwa moja  Dan Welbeck alikuwa wa kwanza kuandika bao la kwa katika dakika ya 61 akifuatiwa na Anderson dakika ya 76 na msumari wa mwisho ukipachikwa katika dakika ya 86 na Wayne Rooney.
kwa maana hiyo Manchester united ina pointi sita na magoli matano.

ASENA WENGER NA SAGA ZAKE


                                           

Kocha wa klabu ya Arsenal, Asena venga anatarijiwa kutangaza ofa juu ya nyota  Eden Harzad toka Lile na Yan M,Via wa Rennes pamoja na Phili Jageka wa Evarton.

Ambaye ambaye sasa kikosi chake kimeanza vibaya ligi kuu ya uingereza baada ya kuanza kwasare na kufungwa mchezo mmoja anataraji kulazimisha suala hili kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Kwa mujibu wa taarifa toka ndani ya klabu hiyo Arsena itatumia kiasi chapaundi milion 17 kwa M, Via napaundi milion 22 kwa Edena Hazrd wakati washika bunduki hao wakiripotiwa kuongeza dau hadi kufukia paundi milion 11 kwaajili ya Jageka,

Baada ya mauzo ya Farbegas Venga analazimika kumsajili Mvia kwaajili ya kukava nafasi ya kiungo haswa baada ya kiungo wa Valencia kuwanjiani kuelekea Chelsea.

                              
Wakati huohuo baadhi ya wadau  wa soka ulimwenguni wakitoa maoni ya juu ya hilo lakini wengi wakimtaka bosi huyo wa kifaransa kusajili haraka wachezaji wenye uzoefu ilikuleta mafaniki katika klabu hiyo.

Kumbuka kuwa bosi wa zamani wa klabu hiyo George Graham amemtaka Vena kusajili vifaa bora hara iwezekanavyo.
Mpaka sasa Arsena imemsajli  Gervinho na Carry Jenkoson huku zikivuma tetesi za Nasri Kuondoka baada ya Farbegas.

                                               
Pia kocha wa Arsenal Arsena Venga amefungiwa  Mechi mbili za klabu bingwa barani ulaya  kwa kosa la kukiunga baadhi ya vipngele vya michuano hiyo ya klabu bingwa barani ulaya.

Huku taarifan toka Kaskazini mwa jiji la London zinasema kuwa Arsenal imetozwa faini ya Uro 10000  kwa kosa la uendeshaji na usimamiaji wa waajiri wake.

Wenga atakosa kusimamia mchezo huo kwa kosa  la kuvuka zaidi ya maramoja  eneo lake  katika benchi la klabu hiyo kwa maana hiyo Venga atakawepo katika mechi ya pili na Udinese.


Wakati huohuo Arsenal imetangaza kumuongeza mshmbuliaji Ryo Miyaichi raia wa Japani katika kikosi kitakacho ivaa Udinese  siku ya Jumatano 
                          

Arsenal ambayo inacheza mchezo wa Play off huku ikiwa na matokeo ya goli moja kwa sifuri yaliyoyapata katika mchezo wake wa kwanza itamtumia Ryo kama sehemu ya kuboresha kikosi chake haswa katika safu ya ushambuliaji 

Bosi wa Arsena Arsena Venga amesema ataingia katika mchezo huo huku akiwa na majeruhi kadhaa pamoja na matumaini ya kumtumia kiungo anayewindwa na Manchester city Samir Nasri.