Monday, August 22, 2011

FARBEGAS MWANZO MZURI




Kiungo wa mpya wa FC Barcelona Cesc Farbegas jana amefuwafurahisha mashabiki wake wa klabu hiyo ya Catalunya baada ya kufunga goli lake la kwanza tangu ajiunge na klabu hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Napoli 

Farbega amesema kwa sasa anamatumaini mapya juu ya ujio wake katika klabu hiyo aliyoitumikia wakati wa utoto wake na kusema atatomsaada wa kutosha kama alivyosaidiwa yeye klabu hiyo.

Hii inadhihirisha kuwepo mianya ya mafanikio kwa nyota huyo kwakua tangu ajiunge na klabu hiyo  amepata mafaniki kwa kutwaa mataji mara mbili.

Ambapo masaa 24 tangu ajiunge ametwaa taji la Super cup dhidi ya Real Madrid na usiku wa jana walitwaa  taji la hisani la Joan Gamper.

Siku ya Ijumaa kule Monaco nchini Ufaransa, Barcelona itaavaana na  Porto FC katika mchezo wa Super cup.

No comments:

Post a Comment