Thursday, August 25, 2011

AVB AMTAKA ALVARO

                              
Bosi wa klabu ya Chelsea Andre Villa Boas maarufu kama AVB anaelekeza nguvu kwa kuitaka saini ya mlinzi wa pembeni wa FC Porto Alvaro Pereira.

Alvaro  mwenye umri wa miaka 25 raia wa Uruguayi amehusishwa na kutaka kujiunga na miamba hiyo ya darajani wiki chache zilizopita ambapo siku ya jumanne Chelsea walianza kuonyesha nia ya  kutangaza Ofa.

Huyo si mchezaji wa kwanza kuwaniwa na AVB bila ya mafanikio tangu ajiunge na Blues akitokea kwa mabingwa wa Ulaya na Ureno kwa ujumla.

Boas anasema kiukweli anamuhitaji nyota huyo lakini hana matumaini ya kufikia makubaliano na uongozi wa Porto juuya usajili wa mlinzi.