Monday, September 12, 2011

SERENA ASUBIRI HUKUMU


                                 
Mcheza tenis maarufu duniani Serena Williams anasubiri kujua kama ataadhibiwa kwa kosa la kumfokea mwamuzi anaejulikana kwa jina Eva Asderaki wakati akicheza na Sam Stosur katika fainali ya tennis ya US Open mjini New york.

Katika fainali hiyo Serena alifungwa na Sam Stosur kwa seti 6-2,6-3 baada ya Williams kuchukulia hatua na mwamuzi huyo wa kigiriki.

Kwa sasa bado anasubiriwa afisa wa pili wa aliyehusika na mwamuzi Brian Earley kama atampa adhabu mshindi huyo wa Grand Slam 13.

Williams, mwenye umri wa miaka 29, tayari anaendelea na adhabu aliyopewa ya miaka miwili, kutokana na kupaza sauti na kulalamika katika mashindano mengine makubwa ya Grand Slam, mwaka 2009.

Lakini Uamuzi wowote utakaochukuliwa dhidi ya Serena Williams bila shaka zitazingatia uzito wa tukio lenyewe alilolifanya.