Friday, September 16, 2011

FERGUSON ALIA NA CHELSEA KATIKA UBINGWA


                        
Kocha wa manchester united sir Alex Fagason amesema klabu ya Chelsea itaipa timu yake changamoto kubwa katika mbio za ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Amesema mbali na timu zote kutoka jiji  la manchester kufanya vizuri katika michezo minne ya kwanza bado kocha cha Chelsea Andre Vila Boas na jeshi lake wana nafasi kubwa ya kule ushindani wa kuponya taji la ligi.
Fagason amesema ndani ya miaka saba sasa michezo na Chelsea inakuwa migumu kiasi kikubwa  na anafikiri mchezo wa jumapili utafuata nyayo hizo kwa kuwa mgumu kupita kiasi kwa kuwa kila mmoja anaamini ndio mwanzo mzuri wa safari ya ubingwa

Aliongeza kuwa Chelsea wana timu yenye uzoefu mkubwa kwa sasa na watafurahia mchezo kama wapo kwao kutokana na umahiri na jinsi walivyojizatiti kushindana.

Fagason ameweka wazi kuwa tendo la kuweka benchi baadhi ya nyota katika mchezo wa klabu bingwa alio ibuka na sare dhidi ya Benfica, alikuwa katika njia panda ya kujua mchezo upi utakuwa mgumu mno.

Katika mchezo huo wa jumapili Fagason anaumiza kichwa kwa wachezaji wake Daren Fretcher, Ji sung Park na Antonio Valencia huenda wasichezo lakini pia Dan Welbeck atakuwemo katika mchezo unaofuata dhidi ya Stoke City baada ya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya Arsenal.