Wednesday, September 14, 2011

EBONY YARAMBA TISA TOKA KWA RUAHA NATIONAL PARK

                                               Hapa wanaulizana baada ya goli sita kuingia

CAVALHO APIGWA PINGU MWAKA MZIMA.


                                              
Mlinzi wa klabu ya Real Madrid Ricaldo Cavalho  amefungiwa kwa muda wa miezi 12 na shirikisho la mpira wa miguu nchini Ureno FPF, kuitumikia timu ya taifa ya Ureno.

Mlinzi huyo wa zamani wa Chelsea mwenye umri wa miaka 33 amefungiwa kwa kosa la kutoka nje ya mazoezi  bila ya maelezo ya msingi baada ya kuambiwa na kocha wake kumwambia kuwa hatoanza katika mchezo wa dhidi ya Cyprus wa kuwania tiketi ya kucheza kombe la ulaya mwaka 2012.

Baada ya tukio la kutoka uwanjani baadae Cavalho alisikika akisema kuwa amechoshwa na timu ya taifa kutokana na kutoheshimiwa na uongozi wa shirikisho na timu hiyo.

Taarifa zandani zinasema kuwa tayari kocha wa Ureno Carlos Manuel Brito Leal Queros, aliekuwa kocha msaidizi wa manchester united alimwambia Cavalho kwamba hana nafasi katika kikosi chake.

Kwa upande wa FPF wamelazika kupunguza ibara ya 21 ya kanuni za timu ya taifa kwa nchi hiyo inayoruhusu adhabu ya miezi 24 kwa mchezaji anaevunja miko ya nidhamu katika timu ya taifa na badala yake wamempa adhabu ya miezi 12.