Thursday, September 8, 2011

HAMMAN KIKAANGONI SEPTEMBER 15


                                  Kamati ya nidhamu na maadaili ya Shirikisho la mpira duniani FIFA itatoa wiki ijayo maamuzi ya rufaa ya aliekuwa mgombea wa urais wa FIFA Mohammed Bin Hamman.

Maamuzi  ya kiongozi huyo wa soka la Asia yatatolewa september 15  ambapo kamati ya rufaa ya shirikisho hilo itakuwa ikilishughulikia suala hilo.

Katika kikao hicho wadau mbalimbali wapo katika hali ya sintofahamu kama Bin Hammaa natahudhulia kikao hicho ama atawakilishwa na wakili wake.

Bin Hamman mwenye umri wa miaka 62 raia wa Qatar ambaye pia alikuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho hilo alivuliwa wadhifa huo kwa na kamati ya maadaili ya FIFA baada ya kukabiliwa na tuhuma za rushwa katika maandalizi ya kuingia katika uchaguzi mkuu wa FIFA ambao Sep Blater aliibuka na ushindi kama mgombea pekee.

Kiongozi huyo pamoja na aliekuwa makamu wa raisi wa FIFA na Shirikisho la mpira barani Amerca CONCACAF, walitajwa kutumia kiasi cha dola milion moja kama hongo walizotoa katika kikao cha Carribean Footbal Union CFU kilichofanyika Trinidadi tarehe 10 mwezi May.

Ili aminiwa kuwa Haman alikuwa akitumia kiasi cha dola elfu arobaini (40.000)  kwa kila shirikisho ili kuongeza kura zake katika kampeni za uraisi wa FIFA