Wednesday, August 24, 2011

ARSENA YAFUZU RASMI KLABU BINGWA.


klabu ya Arsenal imefuzu kushiriki klabu bingwa barani ulaya kwa kuingia hatua ya makundi  mara baada ya kuichapa Udinese magoli mawili kwa moja katika mchezo uliochezwa nchini Italia katika uwanja. Comunale Friuli
udinese ilikuwa ya kwanza kupta bao katika dakika ya 39 kupitia mshambuliaji wake Antonio Dinatale kabla ya dakika ya 55 Robin Van parse kuunganisha krosi safi ya Gervinho na kuipatia Arsenal goli la kusawazisha.


dakika ya 70 Theo walcot alionyesha umahiri wake wa kukimbia na kufunga goli la pili na ushindi lakini kabla ya goli hilo Udinese walipata Penalt ilyopigwa na Dinatale na kipa wa Arsenal kupangua mpira.

kesho shirikisho la soka barani ulaya linafungua ile draw ya makundi ya michuano hiyo ya klabu bingwa.
TIMU NYINGINE ZILIZO FUZU HATUA HIYO NI HIZO ZILIZOWEKWA KIVULI

 
 
Aggr. BATE 3 - 1 Sturm Graz Tue 16/08/11
 Wed 24/08/11 Sturm Graz 0 - 2 BATE

Aggr. Benfica 5 - 3 Twente
 Tue 16/08/11 Twente 2 - 2 Benfica 
 Wed 24/08/11 Benfica 3 - 1 Twente
 
Aggr. Udinese 1 - 3 Arsenal

 Aggr. APOEL 3 - 2 Wisła Kraków

  Aggr. Genk  P 2 - 1 Maccabi Haifa


Aggr. Villarreal 3 - 1 OB
 Wed 17/08/11 OB 1 - 0 Villarreal 

 Aggr. Bayern München 3 - 0 Zürich

CHELSEA YA MSAJILI MATA


Klabu ya Chelsea imakamilisha usajili wa kiungo wa Valencia Juana Mata kwa kumpa mkataba wa miaka mitano
Siku ya jumatatu Valencia na chelsea zilifikia makubaliano na kuuziana nyota huyo nmwenye umri wa miaka 23 kabla ya kufanyiwa vipimo vya afya.

Mpaka jioni ya leo  Chelsea imekamilisha ndoto za nyota huyo kucheza ligi kuu ya uingereza baada ya bosi wa Arsenal Asena Venga kubipu kumsajili kiungo huyo.

Mata akizungumza kupitia mtandao wa Chelsea amesema kuwa Valencia ni klabu kubwa lakini anafuraha kujiunga na klabu kubwa zaidi ya klabu yake ya zamani.

Nyota huyo anakwenda kujiunga na nyota wapya wa klabu hiyo kama Romel Lukaku pamoja na Thobias Cotoo ambao wote wamejiunga na Chelsea msimu huu.

Ujio wa mata ndani ya Chelsea umewasha taa nyekundu kwa kiungo mkongwe wa klabu hiyo Frank Lampard ambaye wanalinga namba katika klabu hiyo.

NASRI NDANI YA NAMBA 19 YA CITY.



Klabu ya Manchester city imetangaza rasmi ukamilisho wa usajili wa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Arsena Samiri Nasri kwa mkataba wa miaka minene. mara baada ya kupasi vipimo vya afya,

Jana klabu hiyo ilitangaza kufikia makubaliano na Gunners na kuepeleka mchezaji kutolewa katika orodha ya nyota watakaojumuika  na Arsena katika mechi ya leo dhidi ya Udinese.

Nasri aliecheza mchezo wa ligi kuu uliozikutanisha Arsena NA liverpool ambapo Arsena ilibamizwa magoli mawili kwa sifuri kwa sasa amekamilisha kile alichokuwa anakihitaji cha kujiunga na klabu nyingine iliapate malipo mazurio zaidi.

Hii itakua faraja kwa Roberto Mancini kwa kumpata kiungo aliekuwa akimtaja kwa kuamini atakuwa muhili wa kutosha katika klabu yake.

Lakini pia kiungo atakae vaa jezi namba 19 mgongoni atakuwa amekata hamu ya mashabiki wa manchester united waliokuwa wanahamu ya kumnasa kiungo huyo wa kifaransa.

Kwabaadhi yamaoni ya wadau na mashabiki wa klabu ya Arsenal ulimwengu wamemtaka mzee Venga kuanza kazi ya kuziba mapengo hayo makubwa mawili likiwemo la Cesc Farbegas lakini wengine wakijiandaa kutafuta timu nyingine

CHEKA NA MAUGO KUSHEREHEKEA IDDI


                                 Maandalizi ya pambano la msumbwi kati Francis cheka na Mada maugo linalotaraji kufanyika siku ya tareh mbili mwezi ujao katika uwanja wa Jamhruri mkoani Morogoro yamekamilika


Akizungumza na shamba la bibi muandaaji wa pambano hilo Kaike siraju amesema pambano hili litakuwa na mapambano kumi ya Utangulizi huku mwadada Asha Ngedele akiwa ni mmoja ya mabondia wa siku hiyo lakini bila ya kusahau burudani ya muziki toka kwa Juma Nature na Afande Sele itakuwepo