Monday, August 29, 2011

KIHEREHERE KIMEMPONA BOLT

                              
Mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt jana aliondolewa katika fainali za mita 100 kwa wanaume katika mashindano ya dunia ya riadha yanayo endelea mjini Daegu, Korea ya Kusini, huku raia mwenzake wa Jamaica, Yohan Blake, akipata dhahabu. 

Bolt ambaye bingwa mtetezi wa dunia aliwashangaza mashabiki wengi wa riadha katika uwanja wa Daegu, alipoondolewa kwa kosa la kuanza mbio kabla kusikia mlio wa bunduki inayowaruhusu kukimbia.

Mara baada ya Bolt kutolewa mjamaica mwenzake Yohan Blake alimudu kumfariji ,wenzake katika mbio hizo mara baada ya kushinda  kwa sekunde 9.92,  huku akimtangulia Mmarekani Walter Dix aliekimbia kwa sekunde 10.08 na bingwa wa dunia mwaka 2003, Kim Collins aliekimbia kwa sekunde10.09.
                               Lakini gumzo limezuka kwa Bolt alietarajiwa kushiriki mbio za mita 200 na mita 100 mara  4 baada ya kuvunja sheria za riadha kwa kuanza kukimbia kabla ya  kuruhusiwa na bunduki ya mwamuzi.

Kwa mujibu wa kanuni  Bolt amevunja kanuni ya  riadha, nambari 162.7, inayo mruhusu mwanariadha kuondolewa kama ataanza mbioo kabla ya mlio huo.

Sheria hiyo mpya ilitangazwa na shirikisho la kimataifa la riadha, IAAF, mwanzoni mwa msimu wa riadha mwaka 2010.

Blake, mwenye umri wa miaka 21 alimsikitikia mwenzake Bolt, ambaye hufanya mazoezi naye,lakini pia amesema kuwa amefurahishwa sana na ushindi huo wa ghafula.

Blake amesema kuwa alihisi angepata ushindi huo kwa niaba ya Bolt ambaye ni rafiki yake.
Collins, mwenye umri wa miaka 35, na alielezea wasiwasi wake kuhusiana na sheria hiyo mpya, baada ya kupata medali yake ya shaba.

Bolt, mwenye umri wa miaka 25, amekuwa akiwika katika mbio fupi miaka michache iliyopita, tangu alipovuma na kuandikisha rekodi katika mbio za mita 100 na 200 katika mashindano ya Olimpiki 2008 na vile vile Roma, kwa kuandika rekodi kwa muda wa sekunde 9.58 na 19.19.

Baadhi ya wanariadha wazoefu wa mbio za mita 100 walikuwa wamekosekana katika fainali hizo za Daegu, wakiwemo wanariadha Asafa Powell, Steve Mullings, Tyson Gay na Muingereza Dwain Chambers ambaye aliondolewa katika nusu fainali, pia baada ya kuanza mbio kabla ya mlio wa bunduki