Tuesday, September 13, 2011

SAMAHANI KUTOKA NJE YA MICHEZO MSIBA UNANIHUSU MIMI NA TAIFA KWA UJUMLA

Maziko ya watu waliofariki kwenye ajali ya meli



Viongozi mbali mbali walijumuika kwa pamoja na wananchi katika kuwaombea dua wananchi waliofariki katika ajali ya kuzama meli ya Mv Spice Islander katika maeneo ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja juzi,sla ya kuwaombea dua maalum iliswaliwa katika viwanja vya maisara mjini Zanzibar jana.
Baadhi ya wananchi walioshiki katika sala na dua maalum wakiwa katika sala ya maiti ya kuwaombe wananchi waliofariki katika ajali ya meli ya mv Spice Islander katika viwanja vya maisara mjini Zanzibar jana.
Maelfu ya wananchi wakimsikiliza Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwahutubia wakati wa dua maalum ya kuwaombea katika viwanja vya maisara Mjini Zanzibar. Foto:  Ramadhan Othman IKulu.

MUANGOLA AWA MISS UNIVERSE

                                                  MREMBO kutoka nchini Angola, Leila Lopes, ametwaa umalkia wa Miss Universe, baada ya kuwashinda wenzake katika shindano lililofanyika mjini Sao Paulo, Brazil.

Mnyange huyo aliacha kuzungumzia historia ya vita nchini kwao, badala yake aligeukia HIV. Mtanzania, Nelly Kamwelu alishindwa kufurukuta.

Akizungumza baada ya kuvikwa taji ya umalkia jijini Sao Paulo, mnyange huyo mwenye miaka 25, alisema "nikiwa Miss Angola, tayari nimefanya mambo mengi kwa jamii."

"Nimefanya kazi mbalimbali za kijamii. Nimefanya kazi na watoto, nimefanyana wapiga vita Ukimwi. Nimefanya kazi ya kuwajali wazee na nitafanya kila niwezalo kwa nchi yangu," alisema. "Nadhani sasa nimekuwa Miss Universe, nitakuwa tayari kufanya zaidi."

Akijibu swali, Lopes alisema hajawahi kuongeza chochote na kwamba, siri yake mafanikio yake ni mambo matatu kulala sana, kuzuia kupata mionzi ya jua na kunywa maji mengi.

Alisema tabasamu lake limekuwa silaha katika mashindano.

Alipoulizwa kuhusu ubaguzi wa rangi kuhusu kutwaa taji hilo, alisema "ubaguzi wowote unahitaji kusaidiwa.

Siyo kawaida kwa karne ya 21 kufikiria hivyo."
Lopes amekuwa mshiriki wa kwanza kutoka Angola kushinda taji hilo.

Mnyange huyo aliwashinda washiriki wenzake 88, na kutwaa umalkia huo, katika mashindano ya 60 ya dunia  ya urembo.

Alirithi umalkia kutoka kwa Ximena Navarrete wa Mexico, aliyetwaa mwaka jana.

"Ahsante Mungu, nimeridhika na jinsi alivyoniumba na sijawahi kubadili chochote," alisema Lopes.

"Ninajielewa mwenyewe kuwa ni mwanamke mwenye uzuri wa ndani. Nilipata ushauri na mwongozo mkubwa kutoka kwa familia yangu na nimekuwa nikizingatia katika maisha yangu yaliyobaki."

Mrembo aliyeshika nafasi ya pili ni Olesia Stefanko wa  Ukraine mwenye miaka 23, na wa tatu ni Priscila Machado wa Brazil.

Mnyange aliyeshika nafasi ya nne ni Miss Philippines na wa tano anatoka nchini China.

Washiriki hao walikuwa pamoja kwa muda wa wiki tatu mjini Sao Paulo, wakijifunza utamaduni hasa ngoma ya samba, kutembelea watoto na kucheza soka ikiwa ni alama kwamba, Miss Universe inafanya kwa mara ya kwanza nchini Brazil.