Friday, September 9, 2011

ALVAREZ KOCHA MPYA COLOMBIA


                            
Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Colombia aliewika na timu hiyo toka mwaka 1983 ametangazwa  kuwa kocha mpya wa Colombia kuchukua mikoba ya Herman Dario Gomez.

Raisi wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Colombia amesema kuwa msaidizi huyo wazamanio wa Dario Gomez ni atakuwa kocha mpya wa timu hiyo ya Colombia.

 Hii kwa Alvarez ni nasafi yake ya pili kukinoa kikosi hicho ambapo  alishawahi kuinoa timu hiyo kwa miaka miwili 

Kwa upande mwingine ametangaza kufarijishwa baada ya kupata nafasi hiyo na anaimani ya kutimiza lengo lake kuanzia sasa.

Alvarez alichezea timu ya taifa ya Colombia katika kombe la dunia la mwaka 1990 na 1994 lakini pia alicheza michezo 101 ndani ya timu ya Colombia.