Wednesday, August 24, 2011

CHELSEA YA MSAJILI MATA


Klabu ya Chelsea imakamilisha usajili wa kiungo wa Valencia Juana Mata kwa kumpa mkataba wa miaka mitano
Siku ya jumatatu Valencia na chelsea zilifikia makubaliano na kuuziana nyota huyo nmwenye umri wa miaka 23 kabla ya kufanyiwa vipimo vya afya.

Mpaka jioni ya leo  Chelsea imekamilisha ndoto za nyota huyo kucheza ligi kuu ya uingereza baada ya bosi wa Arsenal Asena Venga kubipu kumsajili kiungo huyo.

Mata akizungumza kupitia mtandao wa Chelsea amesema kuwa Valencia ni klabu kubwa lakini anafuraha kujiunga na klabu kubwa zaidi ya klabu yake ya zamani.

Nyota huyo anakwenda kujiunga na nyota wapya wa klabu hiyo kama Romel Lukaku pamoja na Thobias Cotoo ambao wote wamejiunga na Chelsea msimu huu.

Ujio wa mata ndani ya Chelsea umewasha taa nyekundu kwa kiungo mkongwe wa klabu hiyo Frank Lampard ambaye wanalinga namba katika klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment