Monday, August 22, 2011

BRAZI U20 WAWASUTA KAKA ZAO



Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana ya Brazil Oscar Do Santos Emboaba aliiwezesha brazil kutwaa ubingwa wa kombe la dunia la vijana chini ya umri wa miaka 20.

katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Nemesio nchini Colombia Oscar alifunga mabao yote, katika  ushindi wa magoli matatu kwa mawili 

makali ya mchezaji huyo yalianza katika dakika ya 5 na 78 ambapo Osca aliemudu kufunga magoli mawili yaliyomaliza dakika 90 kwa sare ya magoli  2 kwa2.

Ambapo magoli ya Ureno yaliyofungwa na dakika ya 9 na la kuongoza lililofungwa katika dakika ya 59 yalitosha kuzipeleka timu hizo katika dakika 30 za nyongeza na hatimaye katika muda huo Oscar alifunga goli la tatu na ushindi katika mchezo huo wa fainali.

Hii ni mara ya tano brazil inatwaa ubingwa dunia wa vijana chini ya umri wa miaka 20 na kutoa mwanga kwa kaka zao ambao wameshindwa kufanya vizuri katika michuano ya Copa Amerca na ile ya kombe la dunia.

No comments:

Post a Comment