Friday, August 26, 2011

JE UNAMJUA MKWE WA MARADONA


                          
                                  SERGIO AGUELO “KUN”
Katika kipindi hiki cha kiangazi ambapo vilabu vingi vimekuwa vikihaha kutafuta nyota watakao wezesha timu zao kufanya vizuri katika michuano mbalimbali kule barani ulaya.

Lakini mtikisiko mkubwa kwa nyota wa kiargentina ulikuwa kwa mshambuliaji wa Atretico Madrid na timu ya taifa ya nchi hiyo anayejulikan kama Sergio Aguelo.

Jina lake kamili ni Sergio Leonel Aguelo Del Castilo maarufu kama Sergio Arguelo kwa jina la utani anjulikana kama (Kun).

Tarehe 02/06/1988 Aguelo alizaliwa katika jiji la Kwimes nchini Argentina, baba mzazi wa Aguero alikuwa ni mtu mwenye Imani ya Kilebanees lakini kwasasa aguelo ni baba wa mtoto mmoja wa kiume anaeitwa benjamini mtoto huyo alizaliwa 19 februaly 2009 katika jiji la Madrid na mkewe anaejulikana kwa jina la  Giania Maradona mtoto wa nguli wa soka nchini Argentina na kocha wa zamani wa Argentina Diego  Almando Maradona.  Kuzali wa mtoto huyo kulimuwezesha Diego Maradona kupata mjukuu wa kwanza wa kiume.
kuzaliwa kwa mtoto kulimfanya Aguelo kukosa siku zipatazo 20 za mazoezi na klabu yake ya Atretico Madrid, lakini pia Aguelo alizuiliwa na mkwewe kwenda kumuangalia mwanae na kumtaka nyota huyo kuendelea kucheza soka kwa kuwa ndio kazi yake.
Lakini uongozi wa Atretico madri haukujali hayo na kutuma salamu za pongezi kwa nyota wao kupata mtoto wa kiume.

Tukiachana na historia hiyo fupi ya maisha yake ya binafsi katika maisha  ya soka, kipaji cha Aguelo kilianza kuzinduliwa mwaka 1997 akiwa na umri wa miaka 9  katika kituo cha soka cha klabu ya Independes ya nchini Argentina na alidumu katika kituo hicho mpaka mwaka 2003 ambapo alipandishwa rasmi katika timu kubwa na kuanza kushiriki ligi kuu ya Argentina yaani First Divison. Ilikuwa ni Julai 5 mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 15 na siku 35 alicheza mchezo wake wa kwanza  dhidi ya klabu Atretico San Lorenzo na Almaro, ambapo alivunja rekodi ya Diego Maradona iliyowekwa mnamo mwaka 1976 kuanza kucheza ligi akiwa na umri mdogo.
                                           
Lakini pia mwaka  november 26 mwaka 2004 Aguelo alianza kuandika kitabu chake cha ufungaji baada ya kufunga goli lake la kwanza na  kusababisha timu yake kuibuka na sare ya magoli 2 kwa 2 dhidi ya Estudiantes De La Plata. Makali yake ya mwanzo yaliamsha imani ya wa Agentina na kuitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Argentina chini ya umri wa miaka 20 hii ilikuwa mwaka 2005

Tarehe 11  september 2005 Aguero alipata umaarufu wa kufunia nyavu baaada ya kuiongoza timu yake katika ushindi wa magoli manne kwa sifuri dhidi ya Racing Club De Alvela. Mwaka 2006  Aguelo alishuhudiwa akitangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari juu ya kutaka kuihama klabu hiyo na kuelekea nchini Hispania.

Ni kweli mwezi May mwaka 2006 aguelo alijiunga na Atretico Madrid kwa dau la paundi milion 23 na kuvunjarekodi ya usajili katika klabu yake Independent.

Ikumbukwe nyota huyo mwezi mmoja baada ya kujiunga na Atretico Madrid aliibua majadiliano baada ya kutumia mikono kufunga goli goli la ushindi katika mchezo dhidi ya Reactivo Hueva ilikuwa 14 October 2006 na aliiongoza Atretico katika ushindi wa magoli  4 kwa 1 Athletic Bilbao kwa kufunga goli lake la pili tangu ajiunge Madrid mchezo huo ulichezwa September 17 mwaka 2007.

March 2008 Aguelo aliendelea kufurahia soka baada kuwa mchezaji bora wa mechi katika mchezo dhidi ya Barcelona mwaka 2008 alipofunga mara mbili na kusababisha goli moja katika ushindi wa magoli manne kwa mawili wa mikwaju ya penati lakini pia Aguelo alifunga magoli muhimu dhidi ya Real Madrid, Valencia, Sevila na Vila Real na kuisaidia Atretico kushiriki Champion League kwa mara ya kwanza baada ya kukosa kushiriki kwa miaka 10 huku ikiwa nafasi ya nne katika ligi kuu ya Hispania.

Katika msimu wa 2008-2009 Aguero kwamara nyingine tena akikuwa mfungaji bora wa klabu hiyo kwa ushirikiano mzuri kati yake na nyota wa Kiuruguayi Diego Forlan.

September 16 mwaka 2008 nyota huyo wa zamani wa Independence alifunga goli lake la kwanza la Ligi ya Mabingwa katika ushindi wa magoli matatu kwa sifuri dhidi ya PSV

Mwaka 2009-10 Aguelo alikuwa katika msimu mzuri tena kwa kufanya makubwa katika ligi kuu ya Hispani na  ligi ya mabingwa haswa pale alipofunga magoli mawili katika sare waliyoipata dhidi ya Chelsea katika uwanja wao wa nyumbani wa Vicente Calderon

Mwaka huo huo wa 2009-2010 Aguelo alisabisha magoli mawili katika ushindi wa magoli  mawili kwa moja dhidi ya Fulham katika michuano ya UROPA LIGI. Lakini pia may 19 Aguelo aliifikisha Atretico katika fainali ya  kombe la Hispania. Ingawa ilikuwa maajabu kwao kwa kufungwa na Sevila katika uwanja waCamp Nou unaotumiwa na Barcelona. 

Agosti 27 mwaka 2010  Aguelo akiwa na kikosi cha Atretico Madrid walitwaa taji la UEFA Supercup dhidi ya Intermilan ambapo aguelo alisababisha magoli yote mawili yaliyofungwa Hose Antonio Reyes.

January 4 mwaka 2011 Atretico Madrid kupitia mtandao wake ilitangaza kuwa Aguero ameongeza mkataba mpya wa miaka minne na ndani ya klabu hiyo na baadeye kutajwa kuwa Nahodha msaidizi wa klabu hiyo akiwa chini ya Diego Forlani

May 23 mwaka 2011 nyota huyo wa kiargentina alitangaza nia ya kutaka kuihama klabu yake ya Atretico Madridi

Miezi miwili baadaye ilikuwa July 28 mwaka 2011 Manchester city ilitangaza rasmi kumsajili mshambuliaji huyo kwa mkataba wa miaka mitano huku akinunuliwa kwa dau la paundi milion 35 mara baada ya kumuwinda kwa muda mrefu huku Atretico Madridi ikiweka vikwazo mbalimbali vikiwemo vya dau la mauzo ya mchazaji huyo.

Katika klabu yake mpya Aguelo amekabidhiwa jezi namba 16 mgongoni tayari kwa kutumikia Manchester city msimu huu.

Kumbuka kuwa Aguelo hakuwemo katika kikosi kilicho anza dhidi ya manchester united katika mchezo wa ngao ya Hisani ambapo kwa ripoti za karibu kutoka Manchester city kuwa Aguelo alikuwa akisumbuliwa na majeruhi.

Mpaka sasa tunavyozungumza Aguelo ni mchezaji halai wa Manchester city ambaye  amefuatwa na nyota wawili wa kifaransa toka klabu ya Arsena ambao ni Gael Clichy na Samiri Nasri lakini pia yupo na Muargentina mwenzake kipenzi cha mkwewe ambaye ni Carlos Tevez.

KATIKA UTUMISHI WA TIMU ZA TAIFA
Aguelo alianza ktumika mwaka 2007 katika kikosi cha Under twenti kilicho shiriki kombela dunia nchini Canada ambapo alianza maajabu yake kwa kufunga marambili katika ushindi wa magoli sita kwa sifuri dhidi ya panama katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi alifunga goli lake la tatu kwa faulo katika mchezo wa tatu dhidi ya Korea Kaskazini na kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Aguelo hakuishia hapo alifunga magoli mawili katika ushindi wa magoli matatu dhidi ya  Poland katika hatua hiyo ya 16  bora na kutinga robo fainali ambapo iliifunga Mexico katika hatua hiyo na baadaye Chile katika fainali na kutinga fainali dhidi ya Jamhuri ya Cheki

Timu hizo zilitoka sare katika hatua ya makundi ambako walikuwa kundi moja na walicheza mchezo wao wa kwanza wa kundi lao.

Lakini kwenye mchezo huo wa fainali Aguelo alifunga mara mbili na kubuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja huku goli la pilia kifunga katika dakika ya 62.

Baadaya kumalizika kwa mashindano hayo AGUELO alitwaa kiatu cha dhahabu kwa kuibuka mfungaji bora mwenye magoli sita katika michuano hiyo na mpira wa dhahabu kama mchezaji bora wa michuano hiyo.
Aguelo hakuishia hapo tu mwaka 2008 aliitwa na kushiriki  katika kikosi cha  Argentina kilicho shiriki michuano ya Olimpic iliyofanyika jijini Beijing nchini China.

Katika michuano hiyo Agosti 19 2008, Aguelo alianza kwa kasi baada ya kufunga magoli  mawili ndani ya dakika tano katika ushindi wa tatu bila wa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Brazil na kukutanza na Nigeria katika fainali ambao Argentina Ilishinda.

Mwaka 2010 Aguelo alichaguliwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kilicho shiriki michuano ya kombe la dunia kule Afrika ya kusini na kucheza mchezo dhidi ya Korea Kaskazini June 12 mara baada ya kupokea nafasi ya Caros Tevez katika dakika ya 75, athari za nyota huyo ziliifanya Argentina kufunga goli dakika chache baadaye.

Alitopasi za magoli katika magoli ya aliyofunga Gunzalo Higuain klablaya Argentina kupoteza mchezo wake wa robo fainali dhidi ya Ujerumani.

Mwaka huu wa 2001 Aguelo aliitwa katika kikosi cha wachezaji 23 watakao iwakilisha  Argentina katika michuano ya Copa Amerca mwaka 2011 ambapo Argentina ilishindwa kufanya vizuri na michuano hiyo kuandaliwa nchini kwao.

Kumbuka kuwa mabingwa  wa Copa Amerca ni uruguayi.

No comments:

Post a Comment