Thursday, September 15, 2011

TAIFA QUEENS MWENDO MDUNDO


                                   
Timu ya taifa ya Netball ya wanawake taifa Queens jana imejisafishia njia ya kutwaa medali baada ya kufunga afrika ya kusini magoli 32 kwa 29  katika muendelezo wa michuano ya all african games.

Taifa queens iliingia katika uwanja wa Zimete huku ikiwa na rekodi mbaya ya kufungwa na uganda magoli 52 kwa 41 katika mchezo wake wa sita wa ligi hiyo inayoendelea nchini msumbiji.

Timu hiyo mpaka sasa imecheza michezo saba imeshinda mitano na imefungwa miwili huku ikiwa na alama 15 na mchezo mmoja uliobaki dhidi ya  Botswana unaochezwa kesho.

Kwa upande mwingine katibu mkuu wa CHANETA Rose Mkisi amevitaka vyama vya mikoa kuafanya taratibu za uchaguzi haraka huku akigusa zaidi mkoani Iringa.

No comments:

Post a Comment