Siku moja baada ya uongozi wa yanga kukaa na viongozi wa matawi kujadili tatizo lililokumbwa na timu hiyo la kupoteza michezo mbalimbali ya ligi kuu ya Tanzania bara.
Akizungumza nami msemaji wa klabu ya yanga Luis Sendeu amesema mbali na kujadili suala hilo kamati ya utendaji ya yanga ilikaa na kujadili suala la mshambuliaji wa timu huyo Jeryson Tegete anaedaiwa kuwa ni mtovu wa nidhamu.
Amesema nikweli tegete amepewa barua ya kusimamishwa mwezi mmoja na ameondolewa moja kwa moja katika kambi ya klabu hiyo.
Baada ya hayo nilizungumza na jerison tegete kuhusu suala hilo amesema hana la kuzungumza kuhusu maamuzi hayo na anliacha kwa viongozi wa klabu hiyo.
Tegete amesemasuala la timu kuharibu nijambo ambalo hutokea katika vilabi mbalimbali ulimwenguni na linaweza kurkebishika.
No comments:
Post a Comment