Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Cammeroun Samuel Etoo,amekiri kuwa uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Anzi Makachkala unamafanikio makubwa na malipo yamemshawishi kujiunga na klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amejiunga rasmi siku ya jumatano mara baada ya kupita katika vipimo vya afya huku mshahara wake ukiwa ni siri.
Lakini taarifa za ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa Etoo atakuwa akilipwa kiasi cha paundi milion 21.8kwa msimu ikiwa sana na bilion 43 na nukta kadhaa.
Usajili wa Etoo kwenda Anzi umeshangaza wadau wengi wa soka barani ulaya kwa kudhani kuwa asingeweza kuhamia Anz kwa kuwa atajificha kisoka.
Etoo amesema mbali na pesa nyingi sio kigezo kikubwa cha kuhamia klabu hiyo bali ameridhika na utaratibu wa uendeshaji wa klabu hiyo
Mbali na hilo nyota huyo amekumbana na safari ndefu za nchi hiyo ya kirusi, baada ya klabu hiyo kufanya mazoezi mjini Mosco huku mechi zao za nyumbani wakicheza mjini Makachkal katika dimba la Degestan Republic, ambapo sawa na umbali wa km 1000 toka mjini Moscow.
SULEYMAN KERIMOV, MMILIKI WA ANZI MAKACHKALA
Klabu ya Anzi inayomilikiwa na Bilionea Suleyman Kerimov imeanzishwa mwaka 1991 nakutwaa taji la kwanza la ligi ya Urusi mwaka 1999
No comments:
Post a Comment