Saturday, August 27, 2011

FARBEGAS MECHI TATU GOLI MBILI NA MATAJI MAWILI


                             
Usiku wa jana kule nchini uafaransa katika uwanja wa Stade Luis unaotumiwa na klabu ya Monaco  kulichezwa mchezo wa fainali ya Super cup uliowakutanisha mabingwa wawili  bingwa wa Uropa ligi na bingwa  Chamipon Ligue ambao ni Barcelona na FC Porto,

Mchezo huo ulio kuwa mzurio na wenye kusisimua huku ukitawaliwa na ufundi mwingi haswa  kwa wachezaji wa Brcelona ulimalizika kwa Barcelona kushinda magoli mwali kwa sifuri.

Dakika ya 39 ya kipindi cha kwanza mshambuliaji mfupi mwenye kasi na chenga za mauzi toka nchini Argentina LEON Messi ali iandikia barca goli la kwanza kabla ya Cesc Farbegas kuandika goli la pili katika dakika ya 89 baaada ya kupokea pasi safi kwa kifua  na kuandika goli hili wa guu lake la kulia.

Cesc farbegas aliesajiliwa na klabu hiyo toka klabu ya  Arsenal ameanza kwa mafanikio ndani ya klabu hiyo kwa kucheza mechi tatu na kufunga magoli mawili huku akiwa tayari amebeba mataji mawili ambayo ni taji la Joan Gamper waliotwaa dhidi ya Napoli na taji la Super waliotwaa dhidi ya  FC Porto.

Kabla ya kutwaa taji hilo la Uefa Super cup kumbuka kwamba Mess alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa michuano ya Uefa champions Ligue mara baada ya kutangazwa kwa makundi ya ligi ya mabingwa barani ulaya. 

Mchezo huo FC Barcelona ilimiliki mchezo kwa asilimia 69 huku Porto wakiwa na 31 lakini mchezo huo ulitawaliwa na kadi mbili nyekundu toka FC Porto na kadi za njano zipztazo nne.

No comments:

Post a Comment