Saturday, August 27, 2011

TOTO YAAMBULIA SARE KWA LYON


                                         
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imeendelea tena leo kwa mechi moja kati ya African Lyon na Toto Africans mchezo uliochezwa katika uwanja wa Azam Stadium Chamazi maeneo ya Mbagala.
Mchezo huo ulikuwa mkali na wakusisimua umewafanya wababe wa Azam Afrikan Lyon kuibuka na sare ya goli moja kwa moja hadi dakika 90 zinamalizika.

Kesho kwenye uwanja huo wa Azam Stadium kutakuwa na mchezo  kati ya JKT Ruvu na Kagera Sugar. huku Mechi nyingine ikitarajiwa kuchezwa Agosti 30 mwaka huu kati ya Moro United na Toto Africans.

Ambapo kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo mechi nyingine mbili zitachezwa Agosti 31 mwaka huu ambapo Mtibwa Sugar itakuwa mwenyeji wa Kagaera Sugar katika Uwanja wa Manungu, Morogoro wakati Villa Squad na Polisi Dodoma zitaumana kwenye Uwanja wa Chamazi, jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment