Thursday, August 11, 2011

FARBEGAS,NASRI WAZIDI KUMLIZA WENGA


                                     
Nahodha wa Arsenal, Cesc Farbegas anaripotiwa kukaribia kumalizia hatua za kujiunga na Barcelona huku Arsenal ikiaminiwa kupokea kiasi cha paundi milion 34. 

Kocha wa Arsenal, Arsene Venga amesema atatumia vyema hazina ya mauzo ya nyota huyo kwaajili ya kutengeza kikosi imara chenye uwezo wa kukabiliana na  changamoto za ligikuu msimu ujao.

Farbegas mwenye umri wa miaka 24 amekuwa muwazi kwa kutoficha dhamira ya kuondoka katika klabu hiyo ya Ashbaton Groves na kuelekea Barcelona ambako alicheza kipindi cha utoto wake akiwa na umri wa miaka 16.

Uhamisho wa Farbegas aliekubali punguzo la mshahara wake atakuwa mchezaji wa pili kama kujiunga na Barcelona katika kipindi cha kiangazi baada ya Alex Sanchez mwezi uliopita.

wakati huo huo Manchester City ipotayari kumsajili Nasri kwa dau la paundi milion 25 huku ikiahidi kumlipa paundi 1.80.000 

Siku ya jumanne Venga alikamilisha usajili usajili wa kiungo chipukizi Alex Oxlade kwa dau la paundi milion 12 huku akitazamiwa kutaka kumsajili Jua Mata toka Valenzia ambaye tayari dau la kwanza la klabu hiyo lime kataliwa

No comments:

Post a Comment