Bosi wa Bayern munich ya ujerumani Jap Henkes amesema hana mpango wa kumsajili mshambuliaji mwingine kwa kuziba pengo la Ivica Olic ambaye ni majeruhi kwa sasa.
Jioni ya jana mkurugenzi wa klabu hiyo ya nchini Ujerumani Karl Heinz amesema Bayern ina mikakati madhubuti ya kufanya marekebisho ya pengo hilo kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Olic ambaye ni raia wa Crotia atakuwa nje kwa muda wa wiki nane kutokana kusumbuliwa na majeraha ya nyonga.
Jap anamatumaini ya hali ya juu kwa kikosi alichonacho na kudai kuwa afikiri kama kukosekana kwa Olic kunaweza kuleta madhara makubwa katika kikosi chake.
No comments:
Post a Comment