Timu ya taifa ya Jamhuri ya kidemokrasia ya congo itacheza na Angola mchezo wa kimataifawa kirafiki uliopangwa kuchezwa Agosti 27 mwaka huu kule nchini Angola.
Mgeni rasmi wa mchezo huo atakuwa ni rais wa Angola Jose Eduardo ambaye siku hiyo atakuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo atakuwa akitimiza miaka 69 huku baadhi ya viongozi wa timu hizo wanasema kuwa mechi hiyo itakuwa ni moja ya maandalizi ya michuano ya CAN mwaka 2012 kule Equatoriol, Guinea.
Siku saba mara baada ya mchezo huo september 4, Angola itaikarisha Uganda katikamchezo wa kufuzu michuano huku Congo ikielekea Dakar kuwavaa simba wa teranga Senegal mchezo utakaochezwa Agosti 3.
Kocha wa Congo maarufu kama Leopard, Robert Nouzaret jana alitangaza kikosi cha wachezaji 24 watakaoshiriki katika mechi hiyo akiwemo Treso Mputu alietoka katika kifungo cha mwaka mmoja cha FIFA.
No comments:
Post a Comment