Wednesday, August 24, 2011

TUTAJITUMA KUIBOMOA ARSENAL



Leo kutakuwa na mchezo UEFA kati Arsenal na Udinese mchezo wa pili wa mchujo wa kuingia katika makundi ya ligi hiyo ya mabingwa.

Kabla ya mchezo huo kocha wa Udinese Francesco Guidolin amesema amejaribu kufanya mikakati kuongeza hali ya kujiamini kwa wachezaji wake ili aweze kushinda katika mchezo huo wa marudiano.

Katika mchezo wa kwanza Udinese ilifungwa goli moja kwa sifuri ndani ya Uwanja wa Emirates.

No comments:

Post a Comment