Wednesday, August 24, 2011
RAJKOVIC ATUA RASMI HUMBARG
Klabu ya Humbarg ya nchini ujerumani imetangaza rasmi kumsajili mlinzi wa Chelsea Slobodan Rajokovic kwaajili ya msimu huu wa Bundersiliga.
Rajokovic mwenye umri wa miaka 22 jioni ya jana alifaulu vipimo vya afya na kusaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo ya kijerumani mchana wa leo. Huku akitarajiwa kuanza kuitumikia klabu hiyo katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya FC Cologne siku ya jumamosi.
Kwaupande wa bosi wa Humbarg Michael Oening amekirti kuanza kumtumia Jokovic haraka na haoni mapungufu yoyote ya kuyaondoa kwa nyota huyo.
Alimsifu kwa kusema kuwa Rajokovic ni mrefu na ubora ambao hawana katika safu ya ulinzi ya klabu yake.
Rajokovic alisajiliwa na chelsea na baadaye kujiunga na PSV kwa mkopo kabla ya kuitumikia FC Twente kwa muda wa miaka miwili na kutwaa ubingwa wa ligi ya uholanzi mwaka 2010.
Nasasa amesema anamipango madhubuti ya kufanya vizuri katika ligi ya bundersiliga kule nchini ujerumani.
Rajokovic ameodheshwa na rafiki yake Eljero Elia ambaye walikua marafiki katika klabu ya FC Twente lakini pia nyota wa zamani wa Chelsea kama Ghokam Tore, Michael Mancienne, Jacob Sala na Jaffrey Bruma ambao wote wamejiunga na ligi ya bundersliga msimu huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment