Monday, August 29, 2011

REDNAP: MODRIC ALIOMBA KUTOPANGWA KATIKA KIKOSI KILICHOIVAA CITY


                          
Bosi wa Tottenham Hotspurs Hery Rednap amesema kuwa kiungo wake Luca Modric aliomba kutopangwa katika kikosi kitakachoivaa manchester city kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa jana.
Rednap amesema kuwa baadae alimtaka mchezaji huyo  acheze mchezo huo kutoka na klabu yake kuandamwa na majeruhi wengi.

Taarifa zinazo vuma huku kocha huyo akihisi kwamba ni kweli kuwa tayari Chelsea imeongeza kitita hadi kufikia paundi milion 40 kwaajili ya nyota huyo wa Kikroshia.
                             
Modrick ana aminiwa kujiunga na Chelsea haraka kabla ya dirishs la usajili kufungwa siku ya jumatano. Hii inadhirisha kuwa  Modric amechoka kukaa katika klabu hiyo.

Lakini Rednap hakushidwa kuzugumzia mustakbali wa timu yake katika ligi kuu ya uingereza kama inavyoendelea
                             

Kwaupande mwingine Rednap amekiri kuwa hana uhakika kama mshambuliaji wake Peter Crouch atabaki  hadi mwisho wa usajili kufungwa 

Hii inatokana na mashabiki wa klabu hiyo kudai kuwa Spurs inataka kumuuza mshambuliaji huyo huku magazeti mbalimbali yakiandika taarifa hiyo.

Lakini taarifa toka ndani ya Stoke city zinasema kuwa Crouch anatarajiwa kujiunga na Spurs kabla ya kufungwa kwa mlango wa usajili.

Aidha tayari mchezaji mmoja wa Tottenham  Hotspurs, Wilson Palacios  amejiunga na Stoke  kwa paundi milion 7, mara baada ya kupita katika vipimo vya afya usiku wa jana.

No comments:

Post a Comment