Shirikisho la soka nchini TFF limesema kesho litakutana na pande zote mbilli kati ya yanga na wadhamini wa ligi kuu ya Tanzania kampuni ya simu ya mkononi kuzungumza ili kumaliza mgogoro unaoendelea kati ya wana jangwani hao kuvaa jassey yenye nembo nyekundu
Yanga wamekuwa wakilalamika kuhusiana na nembo hiyo kuwa hawawezi kuvaa jezi yenye rangi ya watani wao wa jadi na kwamba katika rangi za wanajangwani hao hakuna rangi hiyo na kufanya hivyo ni kinyume na taratibu zao.
Afisa habari wa TFF Boniface wambura amessema kuwa wanacho kifanya wao ni kufaata kanuni za ligi kuu na kwamba kwa yanga na Vodacom kukubaliana wabadili rangi kutoka nyekundu kuwa nyeusi ni kukiuka kanuni hizo
TFF YATAJA VIINGILIO VYA STARS
Viingilio kwa ajili ya mechi ya mchujo kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon kati ya Taifa Stars na Algeria vitakuwa kama ifuatavyo;
Viti vya kijani ni sh. 3,000, viti vya bluu sh. 5,000, viti vya rangi ya chungwa sh. 7,000, VIP C sh.10,000, VIP B sh. 20,000 na VIP A sh. 30,000. Na tiketi zitaanza kuuzwa Septemba Mosi mwaka huu.
Taifa Stars ambayo tayari kambini tangu jana (Agosti 28 mwaka huu) imeendelea na mazoezi Uwanja wa Karume ambapo wachezaji wote wa ndani waliripoti jana mchana na kuanza mazoezi jioni.
Wachezaji toka nje ya Tanzania waliofika jana usiku ni Abdi Kassim na Dan Mrwanda kutoka Vietnam na Mbwana Samata kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Athuman Machupa (Sweden), Henry Joseph (Norway) na Idrisa Rajab (Kenya) wameingia jioni ya leo.
Nizar Khalfan wa Vancouver Whitecaps ya Canada atakuwa mchezaji wa mwisho kuripoti kambini ambapo atawasili nchini kesho saa 5.15 usiku kwa ndege ya PrescisionAir akitokea Nairobi.
TWIGA YAONDOKA KESHO
Timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twigs Stars) inayoondoka Agosti 31 mwaka huu kwenda Maputo nchini Msumbiji kwenye michezo ya All Africa Games itakayofanyika nchini humo kuanzia Septemba 3-18 mwaka huu itaagwa kesho (Agosti 30 mwaka huu).
Twiga Stars wataagwa saa 6 mchana kambini kwao hoteli ya Itumbi iliyopo Magomeni Mwembechai, Dar es Salaam tayari kwa kuondoka nchini.
Wakati huo huo Kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza majina ya wachezaji 16 watakaokwenda Maputo.
Wachezaji hao ni Sophia Mwasikili, Fatuma Omary, Mwanaidi Tamba, Fatuma Bashiri, Mwajuma Abdallah, Asha Rashid, Mwanahamisi Omari, Pulkeria Charaji, Ester Chabruma, Zena Khamis, Fridian John, Fatuma Mustafa, Ettoe Mlenzi, Ftuma Khatib, Maimuna Said na Mwapewa Mtumwa.
Viongozi watakaofuatana na timu hiyo ni Mkwasa, kocha msaidizi Nasra Mohamed, daktari wa timu Dk. Gania Seif wakati Meneja wa timu hiyo ni Furaha Francis.
Aidha mkwasa amesema timu imejiandaa vya kutosha hakuna kisingizio kinachobaki ni wachezaji wenyewe kuonyesha kile walichofundishwa na walimu
Akizungumzia sababu ya kwenda katika michuano hiyo bila ya kuwa na mechi za kirafiki Mkwasa amesema mechi ambazo walicheza COSAFA zitawasaidia kufanya vizuri na maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo
Mechi ya kwanza ya Twiga Stars itakuwa Septembe 5 mwaka huu dhidi ya Ghana wakati ya pili dhidi ya Afrika Kusini itachezwa Septemba 8 mwaka huu. Twiga Stars itacheza mechi yake ya mwisho katika hatua ya makundi Septemba 11 mwaka huu dhidi ya Zimbabwe.
KIM ATAJA 30 WA TIMU YA TAIFA YA VIJANA.
Wakati huohuo, Kocha wa timu za vijana Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 30 wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kwa ajili ya mazoezi mwezi ujao.
Wachezaji walioitwa ni Saleh Ally (TSA), Jackson Wandwi (Azam), Hassan Kessy (Mtibwa Sugar), Khamis Mroki (Mtibwa Sugar), Yassin Mustapha (Polisi Dodoma), Andrew Kasembe (Moro United), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Ally Teru (Simba), Said Ruhava (Kagera Sugar), Samuel Mkomola (Azam), Frank Damayo (JKT Ruvu), Omega Seme (Yanga), Atupele Green (Yanga), Thomas Ulimwengu (ABC Sweden) na Jerome Lambele (Moro United).
Wengine ni Simon Msuvan (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Alex Joseph (Majimaji), Ibrahim Rajab (Azam), Renatus Patrick (Polisi Dodoma), Abdallah Kilala (AFC), Rajab Zahir (Moro United), Amani Kyata (TSA), Edward Shija (Simba), Alfred Amede (Russia), Khelf Hassan (Kenya), Emily Mgeta (TSC Mwanza), Ramadhan Salum (Simba), Frank Sekule (Simba) na Hassan Dilunga (Ruvu Shooting).
Kim amesema milango ipo wazi kwa wachezaji wengine kuingia katika kikosi hicho popote watakapopatikana kikubwa wawe na uwezo
Sambamba na hilo kime ametangaza program yao itakavyokuwa na nini watafanya katika kipindi hichi kuanzia sept hadi Decemba mwaka huu
No comments:
Post a Comment