Monday, August 29, 2011

WENGER ASEMA AMEDHALILISHWA


                           
Mara baada ya kichapo cha mbakaji cha magoli  8 kwa 2 bosi wa Arsenal,Arsene Venga amesisitiza kuwa bado anamikakati ya kusajili wachezaji wa tatu haraka iwezekanavyo kabla ya kufungwa kwa milango ya usajili Agosti 31 mwaka huu.

Kocha huyo mwenye sifa za ubahili anatarajiwa kumsajili mshambuliaji wa south Korea Park Chu Young huku akitafuta mshambuliaji  na kiungo mmoja.

Amesema kwa sasa wanapesa za kutosha za kusajili wachezaji wazuri nakutafanyika hilo kama nyota hao watapatikana kwa haraka zaidi.

Katika msimu uliopita Wenga alisajili bila ya mafanikio baada ya kumsajili mshambuliaji wa Bordaux Mourin Chamack ambapo katika kipindi hiki cha kiangazi imewauza nyota  mahili wa klabu hiyo Cesc Farbegas na Samir Nasri.

Katika mahojiano mara baada ya mchezo dhidi ya United Venga amekiri kuwa kipigo alichokipata jana ulikuwa ni udhalilishaji wa mashabiki, wachezaji pamoja na uongozi wa klabu hiyo.

Kikosi cha Arsena jana kilicheza mchezo wa tatu wa ligi hiyo na kufungwa michezo miwili na kupata sare moja huku ikiwa na pointi moja katika msimamo wa ligi kuu ya uingereza.
Lakini Venga amesisitiza kutokaa kimya na ataendelea kuhimiza vijana wake kupambana katika ligi hiyo.

WAKATI HUOHUO
Mlinzi wa kushoto wa Arsenal Armand Traole  amefanyiwa vipimo vya afya jumatatu ya leo tayari kujiunga na klabu ya Queen Park Rangers iliyopanda daraja msimu huu.

Nyota huyo wa kifaransa mwenye umri wa miaka 21 ambaye ni zao la kituo cha Arsenal alishindwa kuonyesha uwezo wa kutosha ndani ya klabu hiyo baada ya kuzidiwa na walinzi kama Ashley cole aliye Chelsea sasa na Gaely Clich aliejiunga na  Manchester wiki mbili zilizopita.

Katika harakati za kutafutiwa nafasi nyota huyo aliuzwa kwa mkpo katika vilabu ya Posmouth Juventus nabaadaye Venga akamrudisha Traore katika kikosi chake.

Katika mchezo wa jana ambao  Arsenal ilifungwa magoli nane kwa mawili traole alianza katika kikosi hicho na sasa Traore anaoneka kuwa njiani kuelekea QPR.

No comments:

Post a Comment