Wednesday, September 14, 2011

DAGLISH AZUNGUMZA NA RILEY KUHUSU PENATI


                                 
Bosi wa klabu ya Liverpool Kenny Daglish amesema kwamba amefanya kikao na mwamuzi Mike Riley aliechezesha mchezo wa jumamosi kati ya Liverpool na stoke city 

Daglish amezungumza na Riley katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo juu ya maamuzi ya penati aliyotoa katika mchezo huo na kusababisha liverpool kufungwa goli moja kwa sifuri, goli lenyewe likiwa na penati hiyo.

Amesema ameelewa maelezo aliypewa na mwamuzi huyo na kusema kuwa hana nafasi ya kuhoji ama kupewa sheria na vipengele alivyotumia kwa kutambua kuwa ile ni kazi yake.

Amesema kwa taratibu za mchezo ni vizuri kuheshimu na kutulia pamoja na kuendelea na mipango mingineyo.
Kwa sasa amesema anaamini kuwa timu yake ipovizuri na anajipanga kwa mchezo wa jumapili dhidi ya Tottenhama katika uwanja wa Whitehart Lane.

No comments:

Post a Comment