Wednesday, September 14, 2011

INIESTA NJE MWEZI MZIMA


                                     
Kiungo wa FC Barcelona Andres Iniesta atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu katika mchezo wa jana dhidi ya AC Milan.

Baada ya nyota huyo kugongana na kuumia katika dakika ya 39 nafasi yake ilichukuliwa na kiungo wa zamani wa Arsenal Cesc Farbegas zikiwa zimesalia dakika sita tu kwenda mapumziko.

Iniesta amejiunga na mlinzi wa klabu hiyo Gerrad Pique na Alex Sanchez aliepata majera ya tai  katika mchezo wa wiki iliyopita dhidi ya Real Sociedad siku ya jumamosi ambao pia ulimalizika kwa sare ya magoli  2 kwa 2

Katika mchezo huo Barcelona iliwekwa katika wakati mgumu na kuonekana si lolote mbele ya timu za italia baada ya kumaliza kwa sare ya magoli 2 kwa 2.

No comments:

Post a Comment