Wednesday, September 14, 2011

PAT RICE ASEMA ARSENAL IMNEANZA KAZI


                                                     
Meneja msaidizi wa Arsenal Pat Rice, anaamini kuwa ya sare waliyopata jana katika mchezo dhidi ya Borussia Dortmund wa Ligi ya Ubingwa wa Ulaya ni muelekeo mzuri wa timu hiyo kuanza kubadilika katika msimu huu 2011-2010.

Rice amesema  kipindi alipouzwa mara baada ya mchezo na kusema kuwa timu hiyo imebadilika sana tu kuliko ilivyokuwa mwanzoni mwa ligi kuu ya uingereza na kudai kudai kuwa siku ya jumamosi ndio wameanza ligi katika mchezo dhidi ya Swansea.

Katika mchezo wa jana Arsena ilionekana kuwa imeshashinda mchezo huo kwa goli la dakika ya 42 lilifungwa na Robin Van parse kwa kazi nzuri iliyofanywa na Theo Walcot.

Lakini dakika ya 88 mchezo huo ulikuja kuota mbawa kwa Arsenal baada ya Borusia Dotmund kusawazisha goli hilo kupitia Ivan Perisic.

Kwa upande wa kocha wa Dortmund Jurgen Klopp amesema timu yake ilistahili kupata sare baada ya jitahada kubwa walizofanya.

No comments:

Post a Comment