Wednesday, September 14, 2011

AVB AWASIFU NYOTA WAKE


                                   
Bosi wa klabu ya Chelsea Andre Vila Boas amefarijishwa na kiwango cha nyota wake Fernando Torres alicho kionyesha katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Bayern Leverkusen.

Katika mchezo wa jana uliochezwa katika uwanja wa Stanford Brigde Chelsea ilishinda magoli mawili kwa sifuri na magoli yote yakisababisha na Fernando Torres kwa jitihada kubwa alizoonesha katika mchezo huo wa kundi E.

David Luiz na Juan Mata walifaidika na kazi ya Torres iliyofanywa katika dakika ya 67 na 90 lakini pia Tores alipewa kadi ya njano katika dakika ya 9 ya mchezo.

AVB amekiri kuwa torres amecheza vizuri na kwa mazingatio lakini anapaswa kuongeza bidii katika staili ya ke ya uchezaji.

atika mchezo huo Boas aliwaweka benchi wachezaji wake kama Nicolas Anelka, Frank Lampard na John Terry, na nafasi zao kuchukuliwa na Mireles Srurrigde na David Luiz. Lakini pia Didier Drogba anatarajiwa kuanza mazoezi  ya pamoja kesho Alhamisi tayari kwa mchezo na United.

Amesema kwa sasa hakuana haja ya kuendelea na kuchunguza vipaji vya wachezaji katika uwanja kilichobaki ni kusonga mbele zaidi haswa kwa mchezo wa jumapili dhidi ya Mchester united katika uwanja wa Old Traford.

Lakini pia amesema anaimani na kikosi chake kuwa kitafanya vizuri siku ya jumamosi katika mchezo huo kwa rekodi nzuri ya jana dhid ya Leverkusern

No comments:

Post a Comment