Tuesday, September 13, 2011

DJOCKOVIC BINGWA US OPEN


                                
Mcheza tenis bora duniani Novak Djokovic amethibitisha ubora wake wa kucheza tenis duniani, baada ya kumshinda bingwa mtetezi wa US Open Rafael Nadal  kwa kunyakua taji hilo kwa mara ya kwanza.

Djokovic raia wa Serbia ambaye ni namba moja kwa ubora duniani, alionesha mchezo wa kuvutia na kushinda 6-2 6-4 6-7 (3-7) 6-1 katika pambano lililochukua muda wa saa nne na dakika 10 katika uwanja wa Arthur Ashe.

Nadal, ambaye alitazamiwa kushinda taji kubwa kwa mara ya 11, sasa amepoteza mechi zote sita alizokumbana na Djokovic mwaka 2011.

Djokovic anashikilia mataji ya Australian Open, Wimbledon na US Open.Mara ya mwisho kwa Djokovic kushindwa na Nadal katika hatua ya fainali ilikuwa miezi 12 iliyopita, lakini sasa kibao kimemgeukia Nadal

No comments:

Post a Comment