Thursday, September 22, 2011

FERGUSON ANAMATUMAINI YA KUMTUMIA RIO FERDINAND

                                       Bosi wa Manchester united Sir Alex Ferguson  anamatumaini ya kumtumia mlinzi wake Rio Ferdinand katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Stoke City.

Mlinzi huyo anesumbuliwa na matatizo ya misuli ya nyuma ya goti alitangazwa kucheza mchezo wa jumapili dhidi ya Chelsea kutoka na hali yake ilivyokuwa ikisomeka kwa jopo la madaktari wa Manchester united lakini ikashindikana kumtumia kwa kutokuwa fiti kisawawa.

Lakini jioni ya leo Fagason ameibuka na matumaini yakumtumia katika mchezo huo wa ugenini utakao pigwa katika uwanja wa Britania Stadium kuanzia majira ya Saa 1 na nusu usiku,

Fagason amesem anajua ugumu wa mchezo dhidi ya Stoke city kwahiyo anajipanga kuimarisha ulinzi ilikujihakikishia nafasi nzuri ya ushindi katika mchezo huo. Na maamuzi yake ni kumtumia mlinmzi huyo wa Leeds United na West ham united kwa hapo zamani,

Amesema rio anaamini kwa asilimia kubwa kuwa Rio atakuwa vizuri kwa mchezo wa jumamosi kwa ushirikiano mzuri wa Phil Jones  huku kukiwa na shaka ya Cris  Smalling kukosa mchezo huo kutoka majeraha ya kifundo cha mguu.

No comments:

Post a Comment