Thursday, September 22, 2011

GERRARD KUIKABILI WOLVES

                                          
Kiungo wa klabu ya Liverpool Steven Gerran anauwezekano wa kuanza kumika katika mchezo wa jumamosi dhidi ya WolvesHamton.

Hayo yamekuja baada ya kiungo huyo kucheza takribani dakika 15 za mchezo akitokea benchi na kuchukua nafasi ya Luis Suarez katika mchezo wa Carring Cup dhidi ya Brighton ulimalizika kwa  Liverpool kushinda magoli mawili kwa moja.

Daglish atakuwa na faraja endelevu ya kumtumia nyota huyo mbali na kauli yake ya awali kuwa kurudu kwa Gerrard sio mchango mkubwa kwa kuwa anawapinzani wengi pindi akiwa uwanjani ikiwa na maana anakamiwa mno.

Katika mchezo wa jana Gerrad aliingia katika dakika ya 75 ukiwa ni mchezo wa kwanza ndani ya uzi mwekundu mara baada ya kukaa nje kwa muda wa miezi sita kwa tatizo la jeraha la nyonga.

Gkwa sasa gerrard anaandaliwa na Daglish kuingizwa katika kikosi cha kwanza huku Daglish akihofia hilo ambapo katika kauli yake ya kiufundi zaidi amesema atamuingiza katika orodha ya wachezaji 18 watakojumuishwa katika mchezo huo wa ligi dhidi ya Wolves.

No comments:

Post a Comment