Thursday, September 22, 2011

RANIERI KOCHA MPYA INTER MILAN


                                   
 Klabu ya Inter milan ya nchini Italia imemuajiri aliekocha wa klabu ya AS Roma Claudio Raniel kuwa kocha wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili wa kuinoa klabu hiyo.

Taarifa toka katika mtandao wa klabu hiyo umeeleza kuwa Inter imemtwaa kocha huyo wa kitaliano mwenye umri wa miaka 53 kama kocha mpya ikiwa siku moja tu mara baada ya alikuwa kocha wa Inter Gian Gasperin kufukuzwa kazi ya kuinoa timu hiyo.

Lakini pia mashabiki wa klabu ya Inter Milan wameonekana kumkaribisha kocha huyo kwa mikono miwili na kumpa baraka zote za kuinoa timu hiyo.

Raniel alikuwa hana timu tangu alipoacha kazi ya kuinoa Roma mwezi wa february mwaka huu na aliwahi kuvinoa vilabu vya Juventus, Valencia,Chelsea, Atretico Madrdi, Fiorentina, Napoli na Cagriari, huku Gasperi akiponzwa na kupoteza michezo mitano ndani ya Inter na kumfanya kufungishwa safari katika klabu hiyo.

Ikumbukwe Gasperin alichukuwa na nafasi ya Leonado alieshindwa kutamba na klabu hiyo aliyoipokea toka mikononi mwa Morinho alietimkia Real Madrid.

No comments:

Post a Comment