Thursday, September 22, 2011

PATO NJE MWEZI MMOJA

                                         
Mshambuliaji  wa AC Milan Alexander Pato atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki nne ikiwa na maana ya mwezi mmoja mara baada ya kuumia nyama za paja,

Pato alipata jeraha hilo jana katika mchezo wa ligi ya Serea A dhidi ya  Udinese ulimalizika kwa sare ya goli 1 kwa 1 ndani ya uwanja wa nyumbani wa Sansiro Giuesepe Meaza.

Katika mchezo huo nafasi ya Pato ilichukuliwa na  El Sharaw alieingia katika dakika ya 21 na kufunga goli la kusawazisha katika dakika ya 64  ya mchezo. Ambapo goli la Udinese likiwa limefungwa na  Antonio Dinatale,

Kwa maana hiyo nyota huyo wa kibrazi atakosa mchezo wa  klabu bingwa barani ulaya dhidi ya Viktori Pizen katika uwanja wake wa nyumbani wa Sansiro.

No comments:

Post a Comment