Thursday, September 22, 2011

MORINHO AKIRI NGOMA NGUMU


                                         
Kocha wa Real Madrid Jose Morinho amekiri kuwa kwa sasa ameshindwa kufanya kile ambacho alikipanga awali katika ligi kuu ya Hispania na kudai kuwa yupo nje ya matarajio.

Kocha huyo alizungumza kabla ya mchezo wake dhidi ya FC Lavante alinadi katika vyombo vya habari kuwa anatafuta pointi 40 za haraka haraka ili kufanikisha hatua ya kutwaa taji la ligi kabla ya milango ya ligo hiyo kufungwa lakini baadaye alijikuta akipoteza mchezo kwa kufungwa goli moja kwa sifuri.

Katika maelezo yake ya kiufundi Morinho amesema kikosi chake hakijacheza vizuri katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo na kuipongeza Racing Santander kwa kuutumia vizuri uwanja wa nyumba hususa kwa kzuia kupita kiasi.

Na katika mchezo wa usiku wa jana ambao Madrid ilkuwa tena ugenini katika uwanja wa Campos ilishindwa kutamba kwa wenyeji wa uwanja huo kwa kutoka sare ya bila ya kufungana.

Tukio hilo liliweza kuwa mwanya kwa FC Barcelona waliocheza majira ya saa 5:00 usiku dhidi ya Valencia lakini matokeo yake mchezo huo ulimalizika kwa sare ya magoli 2 kwa 2,

Katika mchezo huo Valencia ilijitahidi kucheza vizuri katika uwanja wake wa nyumbani wa Mestara kiasi ambacho umakini ungeongezeka  Valencia wangeibuka na ushindi mbali na Barcelona kuonekana ikifanya kazi yake ya kwaida kutawala katika umiliki wa kabumbu katika kiwanja,

Matokeo hayo ya jana yamekabiza ligi hiyo kuendelea kluongozwa na Valencia kwa Idadi ya pointi 10 nyuma ya Malaga na Real Betis zenye pointi 9,

No comments:

Post a Comment