Thursday, September 22, 2011

MULUMBU ATUNDIKA DALUGA MAPEMA


                                         
Kiungo wa timu ya taifa ya Congo Yousuf Mulumbu ametangaza rasmi kujiuzulu kucheza soka la kimataifa na kuanza kudili zaidi na klabu yake ya Westbromwhich ya nchini England,

Taarifa toka katika chama cha mpira wa miguu nchini Congo FECOFA kimetangaza kupkea barua ya nyota huyo inayoelezea taarifa hiyo ya kujiuzulu soka la kimataifa kwa upande wa ti mu yake ya taifa.

Katika barua yake  Mulumbu mwnye umri wa miaka 24 amesema  kama ifuatavyo, najua kama ni jambo la kusikitisha kwa mashabiki wa soka nchini Congo na naomba uongozi utambue kutokana na maamuzi yangu binafsi nimeamua kustaafu kucheza soka la kimataifa  na kujuhusisha na majuku ya klabu yangu zaidi, na maamuzi haya yamechukua nafasi ya kubwa kujadiliwa na familia yangu pamoja na washauri wangu wa kiafya,

Kwa upande wa katibu mkuu wa shirikisho la mpira nchini Congo Ediba Elonga alizungumza kupitia vyombo vya habari kuwa wapeokea barua hiyo lakini hawajapata nafasi ya kukaa na kujadili juu ya sula hilo ila afikiri kama kuna nafasi ya kumlazimisha mchezaji kuendelea kucheza kama mwenyewe hana nia hiyo tena,

No comments:

Post a Comment