Friday, September 9, 2011

GARRY COOK AJIUZULU MANCHESTER CITY


                                      
Mkurugenzi wa mtendaji wa manchester city Gary Cook amejiuzulu baada ya kubainikia kwa tuhuma zinazo mkabili za kuudhihaki ugonjwa wa kansa unaomsumbua mama mzazi wa mchezaji wa klabu hiyo Nedum Onuoha raia wa Nigeria anaecheza kwa mkopo klabu ya Sunderland kwa sasa.

Taarifa toka katika mtandao wa Manchester city zinasema baada ya kubainika kwa tuhuma hizo kuwa ni zakweli bodi ya Manchester city ilikubali kuachia ngazi kwa mkurugenzi huyo huku mwenyekiti wa City Khaldoom Al- Mubarak akimuomba radhi mama na wakalan wa mchezaji huyo Dr Onuoha.

Katika kipindi kilichopita wakala Nedam Onuoha ambaye ni mama yake, Dr Onuoha aliandika ujumbe kwa Cook na Marwood kuwa hatoweza kufanya mazungumzo juu ya mwanaye kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa  wa kansa.

Baadaye alipokea ujumbe wa barua pepe toka kwa Cook uliokuwa na maneno ya kuudhihaki ugonjwa wa mama huyo wa kinigeria

Mwenyekiti wa bodi Khaldoom AL Mubarak amesema Garry Cook amefanya kazi kwa muda wa miaka mitatu na amefanya kazi vizuri lakini kwa kubainika kwa tuhuma hiyo hakuna hukumu zaidi ya kuachia madaraka aliyonayo na amefanya jambo la busara kuachia madaraka.

No comments:

Post a Comment