Kocha wa Chelsea ameonekana kama anahitaji kushusha kiwango cha mshambuliaji wake, Fernando Tores, Mara baada ya mshambuliaji huyo kuonekana butu tangu ajiunge na klabu hiyo mwezi january katika kipindi cha dirisha dogo.
Hayo yamekisiwa baada ya kocha wa timu ya taifa ya Hispania Vicent De Bosque, kumwambia Torres kama anataka kupata nafasi katika kikosi cha timu ya taifa ajitahidi kufanya vizuri katika kikosi cha timu yake ili aweze kupata nafasi.
Torres mwenye umri wa miaka 27, alinunuliwa na Chelsea kwa paundi milion 50 akitokea Liverpool huku akiwa na wakati mgumu katika suala la ufungaji ambapo mpaka sasa amefunga goli moja katika michezo 17 aliyocheza akiwa Chelsea.
Alipokuwa Liverpool Torres alicheza michezo 102 na akafunga magoli 65 katika michezo yote aliyocheza.
Lakini bosi wake, Andre Vila Boas, AVB amesema anaimani kuwa Torres ataendelea kuchangia katika kikosi cha kwanza cha Chelsea na atarudi katika nafasi yake ya kawaida ya kufunga magoli.
AVB amesema sifa ya mshambuliaji sio kufunga magoli tu na kutengeza nafasi za ufungaji ni sehemu ya ushambuliaji katika timu.
No comments:
Post a Comment