Mlinzi mpya wa klabu ya Arsena Per Matersacke hanaimani kama atakuwa bora zaidi ya beki wa zamani wa klabu hiyo na timu ya taifa ya England, Tony Adams.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 26 amesema Adams sio mtu anayetangazwa sana na kuonyeshwa katika vituo mbalimbali vya televison lakini ni beki ambaye alikuwa mfano ndani ya Arsenal na dunia kwa ujumla.
Alizungumza hayo katika mtandao wa Arsenal amesema alikuwa akimshuhudia Adams akifanya vitu vikubwa kipindi yeye ana umri wa miaka 12 akiwa hana atadalili za kucheza kama Adams.
Adams mwenye umri wa miaka 45 sasa, ndio mchezaji pekee alieanza kucheza klabu hiyo toka katika kituo cha Arsenal mwaka 1980 na kupandishwa katika timu ya wakubwa mwaka 1983 na kumaliza maisha yake ya soka mwaka 2002 na kuweka rekodi Arsena kwa muda wa miaka 22 bila ya kuhama.
Adams alicheza mechi 504 ndani ya Arsena na kufunga magoli 32 mashindano yote aliyocheza.
Lakini pia Adams alitwaa mataji manne ya ligi kuu. Mawili ya FA Cup na kombe la ligi mara mbili mataji yote hayo alichukua akiwa na bosi wa sasa Arsene Venga.
Kutokana na vigezo hivyo Martesakar anaimani ya kuwa ataongeza kipaji chake na atapata mafanikio ya juu zaidi katika soka akiwa na klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment