Friday, September 16, 2011

GUADIOLA AKATA TAMAA NA UBINGWA.


                                         
Kocha wa Barcelona Pep Guadiola amesema timu yake inauwezekano wa kumaliza msimu bila ya taji lolote lile.
Amesema hawezi kutoa ahadi kama atwaa mataji huku akidai kukaa kimya kwa hadi pale mashindano yote yatakapo malizika

Kauli hizo zimekuja baada ya kikosi cha kocha huyo maarufu kwa kuvaa vimodo zimekuja baada ya kuambulia sare mbili ambapo sare ya kwanza aliipata katika mchezo wa Ligi ya Hispania dhidi ya Real Sociedad na nyingine katika klabu bingwa barani ulaya dhidi ya AC Milan ambapo pote walitoka kwa idadi ya magoli mawili kwa mawili.

Jumamosi ya kesho mabingwa hao watetezi wa ligi ya Hispania watajitupa uwanjani kumenyana na Osasuna katika uwanja wao wa nyumbani wa Camp Nou.

Tukiwa bado nchini Hispania kiungo mshambualiaji wa Real Madrid Cristian Ronaldo yupo mashakani kuingia uwanjani siku ya jumapili kwavaa wanajeshi Lavante FC katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania maarufu kama Laliga.
Mashaka hayo yamekuja baada ya nyota huyo kuumia kutokana rafu aliyochezewa katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Daynamo Zagreb katikati mwa wiki hii

Mchezo huo uliomalizika kwa  Madrid kushinda goli moja kwa sifuri ulipelekea nyota huyo kutoa taarifa kwa mashabikiwa Real Madrid kwamba wachezaji wa Zagreb walikuwa na hasira naye kipindi yupo uwanjani.
Taarifa toka ndani ya miamba ya BLANCOS zinasema kuwa nyota huyo anatakiwa kufanyiwa vipimo vya mwisho kabla ya morinho kutaja kikosi kitakachocheza na FC Lavante.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 26 aliejiunga na klabu hiyo kwa dau la paundi milion 80 akitokea manchester united amenza msimu huu wa 2011-2012 kwa kufunga magoli manne katika michezo miwili ya ligi.

No comments:

Post a Comment