Shirikisho la soka nchini TFF Limeutaka uongozi wa klabu ya yanga kuwachukulia hatua za kikatiba kwa wanachama na wadau wa klabu hiyo ambao wanapeleka masuala yamichezo katika mahakama za kisheria haraka iwezekanavyo vinginevyo litawachukulia hatua.
Kauli hiyo imetolewa leo baada ya kamati ya Shera katiba maadili na hadhi ya wachezaji iliyokutana Septemba 3 mwaka huu kujadili suala la mgogoro wa kikatiba uliopo ndani ya klabu ya yanga baada ya kupokea nyaraka zilizowasilishwa mbele ya kamati hiyo
Mwenyekiti wa kamati ya sheria, katiba, maadili na hadhi ya wachezaji Alex Mgongolwa amesema kamati imefikia maamuzi hayo kutokana na ukweli kuwa madai ya kutaka kuondolewa uongozi wayanga kwa kutumia katiba ya wadhamini ya mwaka 1968 iliyosajiliwa 1971 siyo halali
Aidha Mgongolwa ameeleza hatua zinazoweza kuchukuliwa kwa mtu au mwanachama wa tff atakaefikisha shitaka mahakamani
No comments:
Post a Comment