Amesema mbali na ushindi huo timu yake imekuwa ikicheza vizuri lakini bado imekuwa ikiruhusu mashambulizi ya hatari ambayo muda wowote huweza yakaleta madhara na yakabadili sura ya soka la England wakti wowote.
Hii ni mara ya pili Capelo anazungumza hayo mara kwanza pale alipomaliza mchezo dhidi ya Bulgalia uliomalizika kwa England kushinda magoli matatu kwa sifuri.Capelo aliwataka wachezaji kuongeza bidii na kutoridhika na matokeo hayo.
Englanda usiku wa jana ilipata ushindi wa goli moja kwa sifuri goli lililofungwa na Ashley Young katika dakika ya 35 ya mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Wimbley jijini London.
Huu ni ushindi wa kwanza ndani ya uwanja Wimbley katika hatua hiyo ya makundi tangu walipoibuka na sare mbili moja toka kwa Switzerland na nyingine dhidi ya Montenego.
..........
Bosi wa Tottenham Hery Rednap anaamini kwamba England itatwaa ubingwa wa ulaya mwaka 2012 kule Poland na Ukrain.
Amesema mwaka 2010 alisema kuwa England itatwaa ubingwa wa dunia lakini ikawa sivyo alivyotarajia kwa sasa anaamini kuwa timu hiyoitatwaa ubingwa wa ulaya.
England maarufu kama the Three Lions jana ilishinda goli moja kwa sifuri na kuongoza kwa kundi G kwa pointi 17 ikiiacha Montenego kwa tofauti ya Pointi sita.
Aidha Rednap aliwazungumzia wachezaji wengi England kwa uwezo mzuri wanaonyesha, akiwemo nyota anayemuwinda Gally Cahill.
Lakini pia kocha huyo amepewa nafasi kubwa na kurithi mikoba ya Capelo endapo kocha huyo ataachia ngazi.
No comments:
Post a Comment