De Bosque mwenye umri wa miaka 60 alianza kukinoa kikosi hicho mwezi july mwaka 2008 alipopokea mikoba ya Luis Arogones na kuanza kwa kuafanya maajabu kwa kuifunga Austria na Swizland lakini pia alitwaa taji la World Cup mwaka 2010 kule afrika ya kusini.
Amesema kwa sasa anaweza kuongeza mkataba wake unaomalizika mwaka 2012 ambapo Hispania itakuwa ni moja ya nchi shiriki ya michuano ya Ulaya itakayo fanyika kule nchini Poland na Ukrain.
Aliongeza kuwa amezungumza na raisi wa shirikisho la mpira nchini Hispania, Angel Maria Vila na katibu mkuu wa shirikisho hilo George Perez na mpaka sasa kila kitu kipo sawa.
Mpaka sasa imejihakikishia kufuzu michuano ya ulaya mara baada ya kuibika na ushindi wa goli 6 kwa 0 dhidi ya Lichtensen huku akibakiza michezo miwili kati Scotland na Jamhuri ya Cherk.
No comments:
Post a Comment