Wednesday, September 7, 2011

MTOTO WA ZIDANE AITWA NA MORINHO


                               Tukiwa bado nchini Hispania mtoto wa kiungo wa zamani wa ufaransa na klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane ambaye mtoto wake anajulikana kama Enzo Zinade.

Ameitwa katika kikosi cha timu kubwa ya Real Madrid kwaajili ya kujaribiwa kwa lengo la kujiunga na timu hiyo mojamoja kwa moja,

 Enzo mwenye umri wa miaka 16 anaecheza nafasi ya kiungo katika timu ndogo ya Real Madrid inayo julikana kwa jina la Los Blancos atakuwa chini ya uangalizi wa kocha wa klabu hiyo Hosee Morinho.
Mwaliko huo unaweza kumfanya nyota huyo kuanza kuitumikia klabu hiyo akiwa na umri mdogo tofauti na alivyojiunga baba yake mwaka 2001.

Kwa sasa baba wa Enzo ambaye ni Zidane ni mkurugenzi wa michezo ndani ya klabu hiyo huku akitolea macho watoto wake katika mchezo wa soka.

Mbali na Enzo watoto wengine wawili wa zidane ambao ni Luca Zidane na Theo Zidane wamo katika kituo cha Real Madrid wakisaka nafasi ya mafanikio katika soka.

No comments:

Post a Comment