Thursday, September 8, 2011

RONALDO ATAKA UBINGWA WA ULAYA AKIWA NA MADRID


                                
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristian Ronaldo amesema anataka kutwaa taji la klabu bingwa ya ulaya na Real Madrid

Mshambuliaji huyo alievunja rekodi ya dunia kwa usajili mwaka 2008 alitwaa taji hilo akiwa na Manchester united kule mjini Moscow nchini Urusi.

Amesema inabidi kushinda mataji muhimu kama La liga na klabu bingwa kwa sababu ndio mataji yanayo pandisha chati hali yako ya kimchezo na mafanikio kwa ujumla.

Kwa sasa anaamini Madrid itatwaa taji la 10 la klabu bingwa ya ulaya baada ya kuukosa msimu uliopita kwa kutolewa katika nusu fainali na FC Barcelona.

Wiki ijayo katika michuano ya klabu  bingwa Real Madrid itaanza na kutimua vumbi na Daynamo Zagreb katika mchezo wa kundi D, huku siku ya Jumamosi ikiikaribisha Getafe katika mchezo wa ligi pale Santiago Bernabeu. 

Siku ya jumanne Rolnado alisema Madrid ni klabu Bora duniani na vilabu vingi vinatamani kufikia level ya klabu hiyo ambapo jana kulikuwa na fununu ya mreno huyo kukataa kufunga milango ya kurudi manchester united.

No comments:

Post a Comment