Thursday, September 8, 2011

DAGLISH AMTETEA ANDY CARROL


                                    
Bosi wa klabu ya Liverpool Kenny Daglish amemtetea mshambuliaji wake Andy Carrol mara baada ya kukaa benchi katika mchezo kati England na Wales,

Hayo yamekuja baada ya kocha wa timu ya taifa ya England Fabio Capelo kumwambia Carol kama anataka kuwa fiti iliaweze kuwa katika kikosi cha kwanza apunguze kunywa pombe.
                        
Daglish amesema afikiri kama mtindo wa maisha unaweza kuwa sababu kwa mchezaji huyo na kudai kuwa kikubwa kinacho muangusha nyota huyo ni kutoka katika majeraha ya goti kwa muda mrefu na sivinginevyo.
Amesema anaamini kuwa Andy ni mzuri na anapokea ushauri kwa kila mtu ikiwa kama sehemu ya mafaniko yake katika soka.
Msimu uliopita Carrol alianza kucheza mechi mbili katika michezo minne aliyocheza ndani ya Liverpool na kufunga mara moja lakini pia alifunga mara mbili katika mchezo dhidi ya City katika ushindi wa magoli 3 kwa 0 .

No comments:

Post a Comment