Thursday, September 8, 2011

INCE AWAWAKIA NYOTA WA ENGLAND


                                       Paul Ince ameishambulia timu ya taifa ya soka ya England, akidai kwamba wachezaji wengi hawatambui ni jambo la fahari kuichezea nchi yao

Amesema kuichezea timu ya taifa ya England ilikuwa na kufikia kilele cha mafanikio ya mchezo wa soka lakini sasa hawajali hilo kwa kuwa kuna klabu bingwa ya ulaya na ligi kuu kwa kuwa zinafuatiliwa na mashabiki wengi.

Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya england ayamekuja baada ra kuchukizwa na uchache wa mabao katika mchezo wa kimataifa wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya ulaya mwaka 2012 kule nchini Poland na Ukrain ambapo England iliibuka na ushindi mdogo wa goli moja kwa sifuri katika uwanja wa nyumbani ilhali ilishatoa sare michezo miwili katika uwanja huo uliop jijini London.

Nyota huyo alieitumikia timu ya manchester united Inter Milan na Liverpool amesema wachezaji wa siku hizi wamekuwa na wakitoa sababu za kuwa majeruhi kuchoka na hata kuugua homa pindi wanapoitwa katika timu zao za taifa iliwaweze kucheza mechi za ligi mwishono mwa wiki.

Laikini pia Ince aliwageukia mashabiki wa England kwa kutoonyesha ushirikiano wa kushangilia kikamilifu pindi England ikiwa uwanjani haswa ilipokuwa ikicheza na Wales na kudai hali hiyo huwafanya wachezaji kuwa na wasiwasi wakiwa uwanjani.

No comments:

Post a Comment